Isaiah 22:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana leo Mwenyezi-Mungu wa majeshi ametuletea mchafuko: Kushindwa na wasiwasi katika Bonde la Maono. Kuta za mji zimebomolewa, mayowe ya wakazi wake yasikika mpaka milimani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, anayo siku ya ghasia, ya kukanyaga, na ya kuogofya katika Bonde la Maono, siku ya kuangusha kuta na ya kupiga kelele hadi milimani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, Bwana wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana leo Mwenyezi-Mungu wa majeshi ametuletea mchafuko: kushindwa na wasiwasi katika Bonde la Maono. Kuta za mji zimebomolewa, mayowe ya wakazi wake yasikika mpaka milimani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote, anayo siku ya ghasia, ya kukanyaga na ya kuogofya katika Bonde la Maono, siku ya kuangusha kuta na ya kupiga kelele mpaka milimani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, anayo siku ya ghasia, ya kukanyaga, na ya kuogofya katika Bonde la Maono, siku ya kuangusha kuta na ya kupiga kelele mpaka milimani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, BWANA wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana leo Mwenyezi-Mungu wa majeshi ametuletea mchafuko: Kushindwa na wasiwasi katika Bonde la Maono. Kuta za mji zimebomolewa, mayowe ya wakazi wake yasikika mpaka milimani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani siku ya mastuko na ya maangamizo na ya machafuko imetoka kwake Bwana Mungu Mwenye vikosi, ikaja Bondeni kwenye Maono, ni siku iliyobomoa maboma, vilio vyake vikasikilika mlimani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana siku ya kutaabika, siku ya kukanyagwa, siku ya fujo inakuja, itokayo kwa Bwana, BWANA wa majeshi, katika bonde la Maono; inabomoa kuta; na kuililia milima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana leo Yawe wa majeshi ametuletea fujo, kushindwa na wasiwasi katika Bonde la Maono. Kuta za muji zimebomolewa. Kilio cha wakaaji wake kinasikilika mpaka kwenye milima.