Isaiah 23:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
(Ni Wakaldayo, wala si Waashuru, waliowaacha wanyama wa porini wauvamie mji wa Tiro. Wao ndio waliouzungushia mji huo minara ya kuushambulia, wakayabomoa majumba yake na kuufanya magofu.)
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama katika nchi ya Wakaldayo, watu hawa ambao sasa hawaonekani kama wapo! Waashuru wameifanya nchi hiyo kuwa mahali pa viumbe wa jangwani. Wamesimamisha minara yao ya kuuzingira, wameziteka ngome zake na kuziacha tupu na kuufanya kuwa magofu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; wamesimamisha buruji zao za vita, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
(Ni Wakaldayo, wala si Waashuru, waliowaacha wanyama wa porini wauvamie mji wa Tiro. Wao ndio waliouzungushia mji huo minara ya kuushambulia, wakayabomoa majumba yake na kuufanya magofu.)
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama katika nchi ya Wakaldayo, watu hawa ambao sasa hawaonekani kama wapo! Waashuri wameifanya nchi hiyo kuwa mahali pa viumbe wa jangwani. Wamesimamisha minara yao ya vita kuuzunguka, wameziteka ngome zake na kuziacha tupu na kuufanya kuwa magofu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazama katika nchi ya Wakaldayo, watu hawa ambao sasa hawaonekani kama wapo! Waashuru wameifanya nchi hiyo kuwa mahali pa viumbe wa jangwani. Wamesimamisha minara yao ya vita kuuzunguka, wameziteka ngome zake na kuziacha tupu na kuufanya kuwa magofu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; wamesimamisha ngome zao za vita, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
(Ni Wakaldayo, wala si Waashuru, waliowaacha wanyama wa porini wauvamie mji wa Tiro. Wao ndio waliouzungushia mji huo minara ya kuushambulia, wakayabomoa majumba yake na kuufanya magofu.)
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itazameni nchi ya Wakasidi! Ndio watu wasiokuwa kabila; kwa hiyo Waasuri walitaka kuigeuza nchi yao, iwe kao la nyama wa porini. Lakini sasa wanaisimamisha minara yao ya kulindia, wakayabomoa majumba ya nchi hii na kuyageuza kuwa mabomoko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; wamesimamisha buruji zao za vita, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
(Ni Wakaldea, wala si Waasuria, waliowaacha nyama wa pori waushambulie muji wa Tiro. Wao ndio waliouzungushia muji huo minara ya kuushambulia, wakabomoa nyumba zake na kuufanya mabomoko.)