Isaiah 23:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya miaka hiyo sabini, Mwenyezi-Mungu atauadhibu mji wa Tiro, nao utarudia kufanya uzinzi kwa kujiuza kwa mataifa yote ya dunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwishoni mwa miaka sabini, Mwenyezi Mungu atatembelea Tiro. Naye Tiro atarudia ajira yake ya ukahaba, na atafanya biashara yake na falme zote duniani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, Bwana ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya miaka hiyo sabini, Mwenyezi-Mungu atauadhibu mji wa Tiro, nao utarudia kufanya uzinzi kwa kujiuza kwa mataifa yote ya dunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwishoni mwa miaka sabini, BWANA atashughulika na Tiro. Atarudia ajira yake ya ukahaba naye atafanya biashara yake na falme zote juu ya uso wa dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwishoni mwa miaka sabini, bwana atashughulika na Tiro. Naye atarudia ajira yake ya ukahaba, na atafanya biashara yake na falme zote juu ya uso wa dunia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya miaka hiyo sabini, Mwenyezi-Mungu atauadhibu mji wa Tiro, nao utarudia kufanya uzinzi kwa kujiuza kwa mataifa yote ya dunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miaka 70 itakapokwisha, Bwana ataukagua mji wa Tiro, uyarudie mapato ya uasherati wake, ukiufuata ugoni katika nchi zote zenye wafalme zilizoko ulimwenguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata itakuwa mwisho wa miaka sabini, BWANA ataizuru nchi ya Tiro, naye atarudi apate ujira wake, atafanya ukahaba pamoja na falme zote za ulimwengu juu ya uso wa dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha miaka hiyo makumi saba, Yawe atauazibu muji wa Tiro, nao utarudia kufanya uzinzi kwa kujiuzisha kwa mataifa yote ya dunia.