Isaiah 23:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Fedha utakayopata itawekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Mji wenyewe hautafaidika kwa fedha hiyo ila wale wanaomwabudu Mwenyezi-Mungu wataitumia kununulia chakula kingi na mavazi mazuri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini faida na mapato yake yatawekwa wakfu kwa Mwenyezi Mungu; hayatahifadhiwa wala kufichwa. Faida zake zitaenda kwa wale wanaoishi mbele za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya chakula tele na mavazi mazuri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa Bwana, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za Bwana, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Fedha utakayopata itawekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Mji wenyewe hautafaidika kwa fedha hiyo ila wale wanaomwabudu Mwenyezi-Mungu wataitumia kununulia chakula kingi na mavazi mazuri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini faida na mapato yake yatawekwa wakfu kwa ajili ya BWANA; hayatahifadhiwa kwa ajili yake binafsi. Faida zake zitakwenda kwa wale wakaao mbele za BWANA kwa ajili ya chakula tele na mavazi mazuri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini faida na mapato yake yatawekwa wakfu kwa bwana; hayatahifadhiwa wala kufichwa. Faida zake zitakwenda kwa wale wakaao mbele za bwana kwa ajili ya chakula tele na mavazi mazuri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Fedha utakayopata itawekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Mji wenyewe hautafaidika kwa fedha hiyo ila wale wanaomwabudu Mwenyezi-Mungu wataitumia kununulia chakula kingi na mavazi mazuri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mapato yake ya uchuuzi na ya uasherati yatakuwa mali za Bwana, hazitalimbikwa, wala hazitawekwa za akiba, ila atakayoyapata kwa uchuuzi wake, watagawiwa wakaao machoni pa Bwana, wapate kula na kushiba, tena wapate kuvaa na kujifunika vema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Feza utakayopata itatakaswa kwa ajili ya Yawe. Hawatalinda feza hiyo lakini wale wanaomwabudu Yawe wataitumia kwa kununua chakula kingi na nguo nzuri.