Isaiah 23:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni nani aliyepanga mambo haya dhidi ya Tiro, mji uliowatawaza wafalme, wafanyabiashara wake walikuwa wakuu, wakaheshimiwa duniani kote?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni nani amepanga hili dhidi ya Tiro, mji utoao mataji, ambao wafanyabiashara wake ni wana wa mfalme na wachuuzi wake ni watu mashuhuri wa dunia?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu taji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni nani aliyepanga mambo haya dhidi ya Tiro, mji uliowatawaza wafalme, wafanyabiashara wake walikuwa wakuu, wakaheshimiwa duniani kote?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni nani amepanga hili dhidi ya Tiro, mji utoao mataji, ambao wafanyabiashara wake ni wana wa mfalme na wachuuzi wake ni watu mashuhuri wa dunia?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni nani amepanga hili dhidi ya Tiro, mji utoao mataji, ambao wafanyabiashara wake ni wana wa mfalme na wachuuzi wake ni watu mashuhuri wa dunia?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu mataji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni nani aliyepanga mambo haya dhidi ya Tiro, mji uliowatawaza wafalme, wafanyabiashara wake walikuwa wakuu, wakaheshimiwa duniani kote?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni nani aliyeukatia Tiro shauri hili? Ulikuwa umegawia wengine taji za kifalme, wachuuzi wake walikuwa wakuu wa nchi, nao waliokuwa wenye maduka walitukuzwa kuliko wengine katika nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni nani aliyefanya shauri hili juu ya Tiro, uliotia watu taji, ambao wafanya biashara wake walikuwa wana wa wafalme, na wachuuzi wake ni watu wakuu wa dunia?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni nani aliyepanga mambo haya juu ya Tiro, muji uliosimika wafalme, wachuuzi wake walikuwa wakubwa, wakaheshimiwa katika dunia yote?