Isaiah 23:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Yeye ndiye aliyeyapanga haya yote. Alifanya hivyo akiharibu kiburi chao na kuwaaibisha waheshimiwa wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndiye alipanga jambo hili, ili kukishusha kiburi cha utukufu wote na kuwanyenyekeza wale wote ambao ni mashuhuri duniani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Yeye ndiye aliyeyapanga haya yote. Alifanya hivyo akiharibu kiburi chao na kuwaaibisha waheshimiwa wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA Mwenye Nguvu Zote ndiye aliyepanga jambo hili, ili kukishusha kiburi cha utukufu wote na kuwanyenyekesha wale wote ambao ni mashuhuri duniani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye alipanga jambo hili, ili kukishusha kiburi cha utukufu wote na kuwanyenyekesha wale wote ambao ni mashuhuri duniani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Yeye ndiye aliyeyapanga haya yote. Alifanya hivyo akiharibu kiburi chao na kuwaaibisha waheshimiwa wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mwenye vikosi ndiye aliyelikata shauri lake, auchafue urembo wote, waliojivunia, awanyenyekeze wote waliotukuka katika nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA wa majeshi ndiye aliyefanya shauri hili, ili kuharibu kiburi cha utukufu wote, na kuwaaibisha watu wa duniani wote pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni Yawe wa majeshi! Yeye ndiye aliyeyapanga haya yote. Alifanya hivyo akiharibu kiburi chao na kuwapatisha haya waheshimiwa wake.