Isaiah 24:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mwezi utaaibishwa, nalo jua litaona aibu kuangaza, kwa kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi atatawala huko Yerusalemu katika mlima Siyoni; ataonesha wazee wa watu wake utukufu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwezi utatiwa haya, nalo jua litaaibishwa; kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni atatawala juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu, tena mbele ya wazee wake, kwa utukufu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa Bwana wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mwezi utaaibishwa, nalo jua litaona aibu kuangaza, kwa kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi atatawala huko Yerusalemu katika mlima Siyoni; ataonesha wazee wa watu wake utukufu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwezi utatiwa haya, nalo jua litaaibishwa; kwa maana BWANA Mwenye Nguvu Zote atawala juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu, tena mbele ya wazee wake kwa utukufu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwezi utatiwa haya, nalo jua litaaibishwa; kwa maana bwana Mwenye Nguvu Zote atawala juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu, tena mbele ya wazee wake kwa utukufu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa BWANA wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mwezi utaaibishwa, nalo jua litaona aibu kuangaza, kwa kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi atatawala huko Yerusalemu katika mlima Siyoni; ataonesha wazee wa watu wake utukufu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo ndipo, mwezi utakapojifunika, ndipo, nalo jua litakapoona soni, kwa kuwa Bwana Mwenye vikosi atakuwa yuko mfalme mlimani kwa Sioni namo Yerusalemu, nako mbele ya wazee wake utakuwako utukufu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa BWANA wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mwezi utafezeheka, nalo jua litapata haya ya kuangaza, maana Yawe wa majeshi atatawala kule Yerusalema katika mulima Sayuni; ataonyesha wazee wa watu wake utukufu wake.