Isaiah 25:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Juu ya mlima Siyoni, Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafanyia watu wote karamu ya vinono na divai nzuri, nyama tamu na mafuta, pamoja na divai safi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Juu ya mlima huu Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ataandaa karamu ya vinono kwa mataifa yote, karamu ya mvinyo wa zamani, nyama nzuri sana na divai zilizo bora sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika mlima huu Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Juu ya mlima Siyoni, Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafanyia watu wote karamu ya vinono na divai nzuri, nyama tamu na mafuta, pamoja na divai safi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Juu ya mlima huu BWANA Mwenye Nguvu Zote ataandaa karamu ya vinono kwa mataifa yote, karamu ya mvinyo wa zamani, nyama nzuri sana na divai zilizo bora sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Juu ya mlima huu bwana Mwenye Nguvu Zote ataandaa karamu ya vinono kwa mataifa yote, karamu ya mvinyo wa zamani, nyama nzuri sana na divai zilizo bora sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na katika mlima huu BWANA wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Juu ya mlima Siyoni, Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafanyia watu wote karamu ya vinono na divai nzuri, nyama tamu na mafuta, pamoja na divai safi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mwenye vikosi atayafanyia makabila yote ya watu karamu ya manono huku mlimani, itakuwa karamu yenye mvinyo kali na vilaji vyenye mafuta ya kiini, nazo mvinyo hizo zitakuwa zimechujwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika mlima huu BWANA wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Juu ya mulima Sayuni, Yawe wa majeshi atawafanyia watu wote karamu ya nyama zenye kunona na divai nzuri, nyama tamu zenye mafuta, pamoja na divai safi.