Isaiah 26:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini waovu hata wakipewa fadhili, hawawezi kujifunza kutenda haki. Hata katika nchi ya wanyofu, wao bado wanatenda maovu, wala hawajali ukuu wako wewe Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa neema yaoneshwa kwa waovu, hawajifunzi haki; hata katika nchi ya unyofu huendelea kutenda mabaya wala hawazingatii utukufu wa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu mbaya ajapofadhiliwa, Hata hivyo hatajifunza haki; Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu, Wala hatauona utukufu wa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini waovu hata wakipewa fadhili, hawawezi kujifunza kutenda haki. Hata katika nchi ya wanyofu, wao bado wanatenda maovu, wala hawajali ukuu wako wewe Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa neema yaonyeshwa kwa waovu, hawajifunzi haki, hata katika nchi ya unyofu huendelea kutenda mabaya wala hawaoni utukufu wa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa neema yaonyeshwa kwa waovu, hawajifunzi haki, hata katika nchi ya unyofu huendelea kutenda mabaya wala hawazingatii utukufu wa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu mbaya ajapofadhiliwa, Hata hivyo hatajifunza haki; Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu, Wala hatauona utukufu wa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini waovu hata wakipewa fadhili, hawawezi kujifunza kutenda haki. Hata katika nchi ya wanyofu, wao bado wanatenda maovu, wala hawajali ukuu wako wewe Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asiyekucha akihurumiwa hajifunzi wongofu. ila katika nchi yenye mambo yanyokayo, huendelea kuyapotoa, lakini utukufu wa Bwana hauoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu mbaya ajapofadhiliwa, Hata hivyo hatajifunza haki; Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu, Wala hatauona utukufu wa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini waovu hata wakipewa rehema, hawawezi kujifunza kutenda haki. Hata katika inchi ya usawa, wao bado wanatenda maovu, wala hawajali ukubwa wako wewe Yawe.