Isaiah 26:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama vile mama mjamzito anayejifungua hulia na kugaagaa kwa uchungu, ndivyo tulivyokuwa kwa sababu yako, ee Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mwanamke mwenye mimba aliyekaribia kuzaa anavyogaagaa na kulia kwa ajili ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa mbele zako, Ee Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na utungu na kulia kwa sababu ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa sisi mbele zako, Ee Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama vile mama mjamzito anayejifungua hulia na kugaagaa kwa uchungu, ndivyo tulivyokuwa kwa sababu yako, ee Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mwanamke mwenye mimba aliyekaribia kuzaa anavyogaagaa na kulia kwa ajili ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa mbele zako, Ee BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mwanamke mwenye mimba aliyekaribia kuzaa anavyogaagaa na kulia kwa ajili ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa mbele zako, Ee bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na uchungu na kulia kwa sababu ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa sisi mbele zako, Ee BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama vile mama mjamzito anayejifungua hulia na kugaagaa kwa uchungu, ndivyo tulivyokuwa kwa sababu yako, ee Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenye mimba akifikisha kuzaa hujipinda na kulia kwa uchungu wake, ndivyo, nasi tulivyokuwa mbele yako, Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na utungu na kulia kwa sababu ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa sisi mbele zako, Ee BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama vile mama mwenye mimba anayezaa analia na kugaagaa kwa uchungu, ndivyo tulivyokuwa kwa sababu yako, ee Yawe.