Isaiah 26:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sisi tulipata maumivu ya kujifungua lakini tukajifungua tu upepo! Hatukupata ushindi wowote kwa ajili ya nchi yetu, hatukuweza kuongeza idadi ya watu katika nchi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tulikuwa na mimba, tuligaagaa kwa maumivu, lakini tulizaa upepo. Hatukuleta wokovu duniani, hatujazaa watu katika ulimwengu huu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tumekuwa na mimba, tumekuwa na utungu, tumekuwa kana kwamba tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wo wote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sisi tulipata maumivu ya kujifungua lakini tukajifungua tu upepo! Hatukupata ushindi wowote kwa ajili ya nchi yetu, hatukuweza kuongeza idadi ya watu katika nchi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tulikuwa na mimba, tuligaagaa kwa maumivu, lakini tulizaa upepo. Hatukuleta wokovu duniani, hatujazaa watu katika ulimwengu huu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tulikuwa na mimba, tuligaagaa kwa maumivu, lakini tulizaa upepo. Hatukuleta wokovu duniani, hatujazaa watu katika ulimwengu huu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tumekuwa na mimba, tumekuwa na uchungu, tumekuwa kana kwamba tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wowote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sisi tulipata maumivu ya kujifungua lakini tukajifungua tu upepo! Hatukupata ushindi wowote kwa ajili ya nchi yetu, hatukuweza kuongeza idadi ya watu katika nchi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tulikuwa na mimba, tukashikwa na uchungu, lakini tulipozaa, ni upepo tu! Hatukuipatia nchi wokovu, wala hawakupatikana wenye kukaa ulimwenguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tumekuwa na mimba, tumekuwa na utungu, tumekuwa kana kwamba tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wo wote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sisi tulipata maumivu ya kuzaa, lakini tukazaa tu upepo! Hatukupata ushindi wowote kwa ajili ya inchi yetu, hatukuweza kuongeza hesabu ya watu katika inchi.