Isaiah 27:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu atautwaa upanga wake mkubwa, mkali na imara, na kuliadhibu dude Lewiyathani joka lirukalo na danganyifu; Mwenyezi-Mungu ataliua joka liishilo baharini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku ile, Mwenyezi Mungu ataadhibu kwa upanga wake, upanga wake mkali, mkubwa na wenye nguvu; ataadhibu Lewiathani yule nyoka apitaye kwa mwendo laini, Lewiathani yule nyoka mwenye kujipinda; atamuua yule mnyama mkubwa wa baharini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika siku hiyo Bwana, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu atautwaa upanga wake mkubwa, mkali na imara, na kuliadhibu dude Lewiyathani joka lirukalo na danganyifu; Mwenyezi-Mungu ataliua joka liishilo baharini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ile, BWANA ataadhibu kwa upanga wake, upanga wake mkali, mkubwa na wenye nguvu, ataadhibu Lewiathani yule nyoka apitaye mbio kwa mwendo laini, Lewiathani yule nyoka mwenye kupindapinda; atamwua joka huyo mkubwa sana wa baharini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku ile, bwana ataadhibu kwa upanga wake, upanga wake mkali, mkubwa na wenye nguvu, ataadhibu Lewiathani yule nyoka apitaye kwa mwendo laini, Lewiathani yule nyoka mwenye kujipinda; atamuua joka huyo mkubwa sana wa baharini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu Lewiathani, nyoka yule mwepesi, na Lewiathani, nyoka yule mwenye kuzongazonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu atautwaa upanga wake mkubwa, mkali na imara, na kuliadhibu dude Lewiyathani joka lirukalo na danganyifu; Mwenyezi-Mungu ataliua joka liishilo baharini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ile Bwana atatokea akishika upanga ulio mgumu na mkubwa na wenye nguvu, amlipishe Lewiatani, ni lile joka limkimbialo; yeye Lewiatani, lile joka la kujizinga kabisa, atamwua pamoja na yule nondo alioko baharini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo, Yawe atakamata upanga wake mukubwa, mukali na imara, na kuiazibu Leviatani, ile nyoka inayoruka na kuzongazonga. Yawe ataua nyoka mukubwa anayeishi katika bahari.