Isaiah 27:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo, kutoka mto Eufrate hadi mpakani mwa Misri, Mwenyezi-Mungu ataipura nafaka yake, nanyi Waisraeli mtakusanywa mmojammoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku ile Mwenyezi Mungu atapura kutoka matiririko ya Mto Frati hadi Kijito cha Misri, nanyi ee Waisraeli, mtakusanywa mmoja mmoja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana atayapiga-piga matunda yake toka gharika ya Mto hata kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo, kutoka mto Eufrate hadi mpakani mwa Misri, Mwenyezi-Mungu ataipura nafaka yake, nanyi Waisraeli mtakusanywa mmojammoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ile BWANA atapura kutoka matiririko ya mto wa Eufrati hadi Kijito cha Misri, nanyi, Ee Waisraeli mtakusanywa pamoja mmoja mmoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku ile bwana atapura kutoka matiririko ya Mto Frati hadi Kijito cha Misri, nanyi ee Waisraeli, mtakusanywa mmoja mmoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena itakuwa katika siku hiyo, BWANA atayapigapiga matunda yake toka gharika ya Mto hadi kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo, kutoka mto Eufrate hadi mpakani mwa Misri, Mwenyezi-Mungu ataipura nafaka yake, nanyi Waisraeli mtakusanywa mmojammoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ile Bwana atayapura masuke yote, kuanzia kwenye lile jito kubwa kufikisha mpaka mtoni kwa Misri. Nanyi wana wa Isiraeli, mtakusanywa mmoja kwa mmoja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena itakuwa katika siku hiyo, BWANA atayapiga-piga matunda yake toka gharika ya Mto hata kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo, Yawe atapepeta ngano yake kutokea kwenye muto Furati mpaka kwenye mupaka wa Misri, nanyi Waisraeli mutakusanywa mumojamumoja.