Isaiah 27:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi, Mwenyezi-Mungu, ni mkulima wake; nalimwagilia maji kila wakati, ninalilinda usiku na mchana, lisije likaharibiwa na mtu yeyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi, Mwenyezi Mungu, ninalitunza, ninalinywesha maji mfululizo. Ninalichunga usiku na mchana ili mtu yeyote asije akalidhuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi, Bwana, nalilinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi, Mwenyezi-Mungu, ni mkulima wake; nalimwagilia maji kila wakati. ninalilinda usiku na mchana, lisije likaharibiwa na mtu yeyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi, BWANA, ninalitunza, nitalinyweshea maji mfululizo. Ninalichunga mchana na usiku ili mtu ye yote asije akalidhuru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi, bwana, ninalitunza, nalinyweshea maji mfululizo. Ninalichunga usiku na mchana ili mtu yeyote asije akalidhuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi, BWANA, nililinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi, Mwenyezi-Mungu, ni mkulima wake; nalimwagilia maji kila wakati, ninalilinda usiku na mchana, lisije likaharibiwa na mtu yeyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi Bwana ni mlinzi wake; mara kwa mara ninaunywesha; kusudi mtu asiuharibu, ninaulinda usiku na mchana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi, BWANA, nalilinda, Nitalitia maji kila dakika, Asije mtu akaliharibu; Usiku na mchana nitalilinda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi, Yawe, ni mulimaji wake; ninalimwangilia maji kila wakati. Ninalilinda usiku na muchana, kusudi lisiharibiwe na mutu yeyote.