Isaiah 27:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Silikasirikii tena shamba hili; kama miiba na mbigili ingelilivamia, mimi ningepambana nayo na kuichoma moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi sijakasirika. Laiti michongoma na miiba ingenikabili! Ningepambana dhidi yake katika vita, ningeichoma moto yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hasira sinayo ndani yangu; Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu, Ningepanga vita juu yake, Ningeiteketeza yote pamoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Silikasirikii tena shamba hili; kama miiba na mbigili ingelilivamia, mimi ningepambana nayo na kuichoma moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi sijakasirika. Hata kama pangekuwepo michongoma na miiba inayonikabili! Ningepambana dhidi yake katika vita, ningeliichoma moto yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi sijakasirika. Licha pangekuwepo michongoma na miiba kunikabili! Ningepambana dhidi yake katika vita, ningeliichoma moto yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi sina hasira ndani yangu; Kama mbigili na miiba ingekuwa mbele zangu, Ningepanga vita juu yake, Ningeiteketeza yote pamoja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Silikasirikii tena shamba hili; kama miiba na mbigili ingelilivamia, mimi ningepambana nayo na kuichoma moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukali sinao tena; kama ningeona mikunju na mibigili, ningeipelekea vita mara moja, niichome moto yote pamoja;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hasira sinayo ndani yangu; Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu, Ningepanga vita juu yake, Ningeiteketeza yote pamoja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Silikasirikii tena shamba hili; kama miiba na michongoma ingelilishambulia, mimi ningepambana nayo na kuichoma kwa moto.