Isaiah 27:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivi ndivyo uovu wa wazawa wa Yakobo utakavyoondolewa, hivi ndivyo dhambi yake itakavyofutwa kabisa: Ataziharibu madhabahu za miungu; mawe yake yatasagwasagwa kama chokaa; Ashera, wala madhabahu za kufukizia ubani hazitabaki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hili, basi, hatia ya Yakobo itafanyiwa upatanisho, nalo hili litakuwa matunda ya utimilizo wa kuondolewa kwa dhambi yake: Wakati atayafanya mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa vipande vipande, hakuna nguzo za Ashera au madhabahu za kufukizia uvumba zitakazobaki zimesimama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivi ndivyo uovu wa wazawa wa Yakobo utakavyoondolewa, hivi ndivyo dhambi yake itakavyofutwa kabisa: ataziharibu madhabahu za miungu; mawe yake yatasagwasagwa kama chokaa; Ashera, wala madhabahu za kufukizia ubani hazitabaki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hili, basi, hatia ya Yakobo itafanyiwa upatanisho, hili litakuwa ndiyo matunda ya utimilizo wa kuondolewa kwa dhambi yake: Wakati atakapoyafanya mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa vipande vipande, hakuna nguzo za Ashera au madhabahu za kufukizia uvumba zitakazobaki zimesimama.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hili, basi, hatia ya Yakobo itafanyiwa upatanisho, nalo hili litakuwa matunda ya utimilizo wa kuondolewa kwa dhambi yake: Wakati atakapoyafanya mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa vipande vipande, hakuna nguzo za Ashera au madhabahu za kufukizia uvumba zitakazobaki zimesimama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivi ndivyo uovu wa wazawa wa Yakobo utakavyoondolewa, hivi ndivyo dhambi yake itakavyofutwa kabisa: Ataziharibu madhabahu za miungu; mawe yake yatasagwasagwa kama chokaa; Ashera, wala madhabahu za kufukizia ubani hazitabaki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo manza zao, wa Yakobo walizozikora, zimefunikwa kweli, nalo hili ndilo pato la kuwaondolea makosa yao: mawe yote ya mahali pa kutambikia miungu wameyaponda kuwa mavumbi kama ya mawe ya chokaa yaliyobunguliwa, nayo mifano ya mwezi na ya jua haikusimikwa tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi ndivyo uovu wa wazao wa Yakobo utakavyoondolewa, hivi ndivyo zambi yake itakavyofutwa kabisa: ataziharibu mazabahu za miungu; mawe yake yatasagwasagwa kama chokaa. Sanamu za Ashera wala mazabahu za kufukizia ubani hazitabaki.