Isaiah 28:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu: “Tazama! Naweka mjini Siyoni jiwe la msingi, jiwe ambalo limethibitika. Jiwe la pembeni, la thamani, jiwe ambalo ni la msingi thabiti; jiwe lililo na maandishi haya: ‘Anayeamini hatatishika.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti. Yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu: “Tazama! Naweka mjini Siyoni jiwe la msingi, jiwe ambalo limethibitika. Jiwe la pembeni, la thamani, jiwe ambalo ni la msingi thabiti; jiwe lililo na maandishi haya: ‘Anayeamini hatatishika.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo hivi ndivyo BWANA Mwenyezi asemavyo: “Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti, yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo hivi ndivyo bwana Mwenyezi asemavyo: “Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti. Yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu: “Tazama! Naweka mjini Siyoni jiwe la msingi, jiwe ambalo limethibitika. Jiwe la pembeni, la thamani, jiwe ambalo ni la msingi thabiti; jiwe lililo na maandishi haya: ‘Anayeamini hatatishika.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Nitazameni! Mimi ndimi niliyeweka jiwe, liwe msingi wa Sioni, nalo ni jiwe lililojulika, ya kuwa litafaa la pembeni kwa utukufu wake, likawekwa la msingi kuwa kama mwamba, ni hili la kwamba: Alitegemeaye hatakimbia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Bwana wetu Yawe anasema hivi: Ninaweka katika Sayuni jiwe la musingi, jiwe ambalo limeimarishwa. Jiwe la pembe, la bei kali, jiwe ambalo ni la musingi imara; jiwe linalokuwa na maandiko haya: Anayeamini hataanguka.