Isaiah 28:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nyinyi msiwe na madharau vifungo vyenu visije vikakazwa zaidi. Maana nimesikia kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameazimia kuiangamiza nchi yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa acheni dharau zenu, la sivyo minyororo yenu itakuwa mizito zaidi. Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, ameniambia habari za maangamizi yaliyoamriwa dhidi ya nchi yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, Bwana wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nyinyi msiwe na madharau vifungo vyenu visije vikakazwa zaidi. Maana nimesikia kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameazimia kuiangamiza nchi yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa acheni dharau zenu, la sivyo minyororo yenu itakuwa mizito zaidi, Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote, ameniambia habari za maangamizi yaliyoamuriwa dhidi ya nchi yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa acheni dharau zenu, la sivyo minyororo yenu itakuwa mizito zaidi. Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, ameniambia habari za maangamizi yaliyoamriwa dhidi ya nchi yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, BWANA wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nyinyi msiwe na madharau vifungo vyenu visije vikakazwa zaidi. Maana nimesikia kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameazimia kuiangamiza nchi yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa acheni kufyoza, vifungo vyenu visikazwe, kwani nchi zote zimekwisha kukatiwa shauri la angamizo, kama nilivyosikia kwa Bwana Mungu aliye Mwenye vikosi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, BWANA wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ninyi musikuwe na mazarau vifungo vyenu visipate kukazwa zaidi. Maana nimesikia kwamba Yawe wa majeshi amekusudia kuiangamiza inchi yote.