Isaiah 28:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
fahari yake inatoweka kama ua linalonyauka; fahari iliyotawala bondeni kwenye rutuba itakuwa kama tini za mwanzo kabla ya kiangazi; mtu akiziona huzichuma na kuzila mara moja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake, uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba, litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno: mara mtu aionapo, huichuma na kuila.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, litakuwa kama tini iliyotangulia kuiva kabla ya wakati wa hari, ambayo, aionapo yeye aiangaliaye, huila mara anapoishika mkononi mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
fahari yake inatoweka kama ua linalonyauka; fahari iliyotawala bondeni kwenye rutuba itakuwa kama tini za mwanzo kabla ya kiangazi; mtu akiziona huzichuma na kuzila mara moja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake, uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba, litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno: mara mtu aionapo, huichuma na kuila.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake, uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba, litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno: mara mtu aionapo, huichuma na kuila.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, litakuwa kama tini iliyotangulia kuiva kabla ya wakati wa joto, ambayo, aionapo yeye aiangaliaye, huila mara anapoishika mkononi mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
fahari yake inatoweka kama ua linalonyauka; fahari iliyotawala bondeni kwenye rutuba itakuwa kama tini za mwanzo kabla ya kiangazi; mtu akiziona huzichuma na kuzila mara moja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lile ua litakalonyauka lingaliko, nao urembo wenye utukufu wake linao, kwa maana liko kilimani juu kwenye bonde lioteshalo sana, lakini litakuwa kama kuyu inayoiva upesi, siku za mavuno zinapokuwa hazijatimia bado; mtu akiiona anaichuma hapohapo, tena ikiwa ingalimo mkononi mwake, amekwisha kuimeza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, litakuwa kama tini iliyotangulia kuiva kabla ya wakati wa hari, ambayo, aionapo yeye aiangaliaye, huila mara anapoishika mkononi mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
utukufu wake unatoweka kama ua linalonyauka; utukufu uliotawala katika bonde kwenye udongo muzuri utakuwa kama tini za mwanzo mbele ya wakati wa mavuno; mutu akiziona anazichuma na kuzikula mara moja.