Isaiah 29:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kwenu nyinyi maono yote haya ni kama ujumbe ulioandikwa katika kitabu kilichofungwa kwa mhuri. Ukimpelekea mtu yeyote ajuaye kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atasema, “Siwezi kukisoma kwani kimefungwa kwa mhuri.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwenu ninyi, maono haya yote si kitu ila maneno yaliyotiwa muhuri katika kitabu. Mkimpa mtu yeyote awezaye kusoma kitabu hiki, nanyi mkamwambia, “Tafadhali kisome,” yeye atajibu, “Mimi siwezi, kwa kuwa kimetiwa muhuri.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na maono yote yamekuwa kwenu kama maneno ya chuo kilichotiwa muhuri, ambacho watu humpa mtu aliye na maarifa, wakisema, Tafadhali ukisome hiki; akasema, Siwezi, kwa kuwa kimetiwa muhuri;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kwenu nyinyi maono yote haya ni kama ujumbe ulioandikwa katika kitabu kilichofungwa kwa mhuri. Ukimpelekea mtu yeyote ajuaye kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atasema, “Siwezi kukisoma kwani kimefungwa kwa mhuri.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana kwenu ninyi, maono haya yote si kitu ila maneno yaliyotiwa lakiri katika kitabu. Kama mkimpa mtu ye yote awezaye kusoma kitabu hiki, nanyi mkamwambia, “Tafadhali kisome,” yeye atajibu, “Mimi siwezi, kwa kuwa kimetiwa lakiri.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana kwenu ninyi, maono haya yote si kitu ila maneno yaliyotiwa lakiri katika kitabu. Kama mkimpa mtu yeyote awezaye kusoma kitabu hiki, nanyi mkamwambia, “Tafadhali kisome,” yeye atajibu, “Mimi siwezi, kwa kuwa kimetiwa lakiri.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na maono yote yamekuwa kwenu kama maneno ya kitabu kilichotiwa mhuri, ambacho watu humpa mtu aliye na maarifa, wakisema, Tafadhali ukisome hiki; akasema, Siwezi, kwa kuwa kimetiwa mhuri;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kwenu nyinyi maono yote haya ni kama ujumbe ulioandikwa katika kitabu kilichofungwa kwa mhuri. Ukimpelekea mtu yeyote ajuaye kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atasema, “Siwezi kukisoma kwani kimefungwa kwa mhuri.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo yote mliyoyaona yakawa kwenu kama maneno ya kitabu kulichofungwa na kutiwa muhuri; kama ajuaye kusoma anapewa na kuambiwa: Kisome hiki! atajibu: Siwezi, kwani kimefungwa na kutiwa muhuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na maono yote yamekuwa kwenu kama maneno ya chuo kilichotiwa muhuri, ambacho watu humpa mtu aliye na maarifa, wakisema, Tafadhali ukisome hiki; akasema, Siwezi, kwa kuwa kimetiwa muhuri;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, kwenu ninyi, maono haya yote ni kama ujumbe ulioandikwa katika kitabu kilichofungwa kwa muhuri. Ukimupelekea mutu yeyote anayejua kusoma, na kumwambia “Unisomee kitabu hiki”, atasema “Siwezi kukisoma kwa sababu kimefungwa kwa muhuri.”