Isaiah 29:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na ukimpa mtu yeyote asiyejua kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atakuambia, “Sijui kusoma.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Au mkimpa mtu yeyote kitabu hiki asiyeweza kusoma na kumwambia, “Tafadhali kisome,” atajibu, “Mimi sijui kusoma.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na ukimpa mtu yeyote asiyejua kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atakuambia, “Sijui kusoma.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Au kama mkimpa mtu ye yote kitabu hiki asiyeweza kusoma na kumwambia, “Tafadhali kisome,” atajibu, “Mimi sijui kusoma.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Au kama mkimpa mtu yeyote kitabu hiki asiyeweza kusoma na kumwambia, “Tafadhali kisome,” atajibu, “Mimi sijui kusoma.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha kitabu hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na ukimpa mtu yeyote asiyejua kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atakuambia, “Sijui kusoma.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama asiyejua kusoma anapewa na kuambiwa: Kisome hiki! atajibu: Sijui kusoma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha chuo hiki apewa mtu asiye na maarifa, akaambiwa, Kisome hicho tafadhali, akasema, Sina maarifa mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na ukimupa mutu yeyote asiyejua kusoma, na kumwambia “Unisomee kitabu hiki”, atasema: “Sijui kusoma.”