Isaiah 29:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana asema, “Watu hawa huja kuniabudu kwa maneno matupu, hali mioyo yao iko mbali nami. Wananiheshimu kulingana na mapokeo ya watu tu, jambo walilojifunza wao wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bwana asema: “Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao na kuniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. Ibada yao kwangu inatokana na maagizo waliyofundishwa na wanadamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana asema, “Watu hawa huja kuniabudu kwa maneno matupu, hali mioyo yao iko mbali nami. Wananiheshimu kulingana na mapokeo ya watu tu, jambo walilojifunza wao wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bwana anasema: “Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao na kuniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. Huniabudu bure, mafundisho yao ni sheria tu walizofundishwa na wanadamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bwana anasema: “Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao na kuniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. Ibada yao kwangu inatokana na maagizo waliyofundishwa na wanadamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walichonacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bwana asema, “Watu hawa huja kuniabudu kwa maneno matupu, hali mioyo yao iko mbali nami. Wananiheshimu kulingana na mapokeo ya watu tu, jambo walilojifunza wao wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akasema: Ukoo huu hunikaribia na vinywa vyao, huniheshimu kwa midomo tu, lakini mioyo yao inanikalia mbali; kwa sababu hii hunicha bure, kwani hufundisha mafundisho yaliyo maagizo ya watu tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walicho nacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana anasema: Watu hawa wanakuja kuniabudu kwa maneno tu, lakini mioyo yao iko mbali nami. Wananiheshimu kulingana na desturi ya watu tu, jambo walilojifunza wao wenyewe.