Isaiah 29:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ole mnaomficha Mwenyezi-Mungu mipango yenu, mnaotenda matendo yenu gizani na kusema: ‘Hamna atakayetuona; nani awezaye kujua tunachofanya?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ole kwa wale wanaoenda kwenye vilindi virefu kumficha Mwenyezi Mungu mipango yao, wafanyao kazi zao gizani na kufikiri, “Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wao wanaojitahidi kumficha Bwana mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ole mnaomficha Mwenyezi-Mungu mipango yenu, mnaotenda matendo yenu gizani na kusema: ‘Hamna atakayetuona; nani awezaye kujua tunachofanya?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ole kwa wale wanaokwenda kwenye vilindi virefu kumficha BWANA mipango yao, wafanyao kazi zao gizani na kufikiri kuwa, “Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ole kwa wale wanaokwenda kwenye vilindi virefu kumficha bwana mipango yao, wafanyao kazi zao gizani na kufikiri, “Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ole mnaomficha Mwenyezi-Mungu mipango yenu, mnaotenda matendo yenu gizani na kusema: ‘Hamna atakayetuona; nani awezaye kujua tunachofanya?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatawapata wao walao njama, kwamba: wamfiche Bwana mashauri yao! Nao wafanyao gizani kazi zao na kusema: Yuko nani anayetuona? Yuko nani anayetujua?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ole kwenu ninyi munaomuficha Yawe mipango yenu, munaotenda matendo yenu katika giza na kusema: Hakuna atakayetuona; nani anayeweza kujua tunachofanya?