Isaiah 29:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi mnafanya mambo kinyume kabisa! Je, mfinyanzi na udongo ni hali moja? Chombo hakiwezi kumwambia aliyekitengeneza: ‘Wewe hukunitengeneza.’ Kilichofinyangwa hakiwezi kumwambia aliyekiumba, ‘Wewe hujui chochote.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mnapindua mambo juu chini, kana kwamba mfinyanzi aweza kufikiriwa kuwa kama udongo wa mfinyanzi! Je, kile kilichofinyangwa chaweza kumwambia yule aliyekifinyanga, “Wewe hukunifinyanga mimi”? Je, chungu kinaweza kumwambia mfinyanzi, “Wewe hujui chochote”?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ninyi mnapindua mambo; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, Yeye hana ufahamu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi mnafanya mambo kinyume kabisa! Je, mfinyanzi na udongo ni hali moja? Chombo hakiwezi kumwambia aliyekitengeneza: ‘Wewe hukunitengeneza.’ Kilichofinyangwa hakiwezi kumwambia aliyekiumba, ‘Wewe hujui chochote.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mnapindua mambo juu chini, kana kwamba mfinyanzi aweza kufikiriwa kuwa kama udongo wa mfinyanzi! Je, kile kilichofinyangwa chaweza kumwambia yule aliyekifinyanga, “Wewe hukunifinyanga mimi?” Je, chungu kinaweza kumwambia mfinyanzi, “Wewe hujui cho chote?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mnapindua mambo juu chini, kana kwamba mfinyanzi aweza kufikiriwa kuwa kama udongo wa mfinyanzi! Je, kile kilichofinyangwa chaweza kumwambia yule aliyekifinyanga, “Wewe hukunifinyanga mimi?” Je, chungu kinaweza kumwambia mfinyanzi, “Wewe hujui chochote?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ninyi mnapindua mambo; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, Yeye hana ufahamu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi mnafanya mambo kinyume kabisa! Je, mfinyanzi na udongo ni hali moja? Chombo hakiwezi kumwambia aliyekitengeneza: ‘Wewe hukunitengeneza.’ Kilichofinyangwa hakiwezi kumwambia aliyekiumba, ‘Wewe hujui chochote.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmepotea kabisa! Uko udongo unaowaziwa kuwa sawa na mfinyanzi? Au kiko kiumbe kiwezacho kumwambia aliyekiumba: Hukunifanya? Au kiko chombo kiwezacho kumwambia aliyekifinyanga: Hujui kitu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ninyi mnapindua mambo; Je! Mfinyanzi ahesabiwe kuwa kama udongo; kitu kilichofinyangwa kimnene yeye aliyekifinyanga, Hakunifinyanga huyu; au kitu kilichoumbwa kimnene yeye aliyekiumba, Yeye hana ufahamu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi munafanya mambo kinyume kabisa! Mufinyanzi na udongo ni hali moja? Chombo hakiwezi kumwambia aliyekitengeneza hivi: Wewe haukunitengeneza. Kilichofinyangwa hakiwezi kumwambia aliyekiumba; Wewe haujui kitu.