Isaiah 29:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu aliyemkomboa Abrahamu, asema hivi kuhusu wazawa wa Yakobo: “Wazawa wa Yakobo hawataaibishwa tena, hawatainamisha vichwa vyao tena kwa aibu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo hili ndilo Mwenyezi Mungu, aliyemkomboa Ibrahimu, analosema kwa nyumba ya Yakobo: “Yakobo hataaibishwa tena, wala nyuso zao hazitabadilika sura tena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, Bwana aliyemkomboa Ibrahimu asema hivi, katika habari za nyumba ya Yakobo; Yakobo hatatahayarika sasa, wala uso wake hautabadilika rangi yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu aliyemkomboa Abrahamu, asema hivi kuhusu wazawa wa Yakobo: “Wazawa wa Yakobo hawataaibishwa tena, hawatainamisha vichwa vyao tena kwa aibu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo hili ndilo BWANA, aliyemkomboa Abrahamu, analosema kwa nyumba ya Yakobo: “Yakobo hataaibishwa tena, wala nyuso zao hazitabadilika sura tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo hili ndilo bwana, aliyemkomboa Ibrahimu, analosema kwa nyumba ya Yakobo: “Yakobo hataaibishwa tena, wala nyuso zao hazitabadilika sura tena.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, BWANA aliyemkomboa Abrahamu asema hivi, kuhusu nyumba ya Yakobo; Yakobo hatatahayarika sasa, wala uso wake hautabadilika rangi yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu aliyemkomboa Abrahamu, asema hivi kuhusu wazawa wa Yakobo: “Wazawa wa Yakobo hawataaibishwa tena, hawatainamisha vichwa vyao tena kwa aibu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hii Bwana alimkomboa Aburahamu, akauambia mlango wa Yakobo: Sasa Yakobo hatapatwa tena na soni, wala uso wake hautamvilia tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, BWANA aliyemkomboa Ibrahimu asema hivi, katika habari za nyumba ya Yakobo; Yakobo hatatahayarika sasa, wala uso wake hautabadilika rangi yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, Yawe aliyemukomboa Abrahamu, anasema hivi juu ya wazao wa Yakobo: Wazao wa Yakobo hawatapata haya tena, hawatainamisha vichwa vyao tena kwa ajili ya haya.