Isaiah 29:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mataifa yote yanayoushambulia mji wa Yerusalemu yatakuwa kama mtu mwenye njaa anayeota anakula lakini aamkapo bado anaumwa na njaa! Au mtu mwenye kiu anayeota kuwa anakunywa, lakini anaamka mdhaifu, bado ana kiu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kama vile mtu aliye na njaa aotavyo kuwa anakula, lakini huamka, bado njaa yake ingalipo, kama vile mtu mwenye kiu aotavyo kuwa anakunywa maji, lakini huamka akiwa anazimia, akiwa bado angali ana kiu. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa makundi yote ya mataifa yanayopigana dhidi ya Mlima Sayuni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mataifa yote yanayoushambulia mji wa Yerusalemu yatakuwa kama mtu mwenye njaa anayeota anakula lakini aamkapo bado anaumwa na njaa! Au mtu mwenye kiu anayeota kuwa anakunywa, lakini anaamka mdhaifu, bado ana kiu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kama vile wakati mtu aliye na njaa aotavyo kuwa anakula, lakini huamka, bado njaa yake ingalipo, kama vile wakati mtu mwenye kiu aotavyo kuwa anakunywa maji, lakini huamka akiwa anazimia, akiwa bado angali ana kiu. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa makundi yote ya mataifa, yanayopigana dhidi ya Mlima Sayuni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kama vile mtu aliye na njaa aotavyo kuwa anakula, lakini huamka, bado njaa yake ingalipo, kama vile mtu mwenye kiu aotavyo kuwa anakunywa maji, lakini huamka akiwa anazimia, akiwa bado angali ana kiu. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa makundi yote ya mataifa yanayopigana dhidi ya Mlima Sayuni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mataifa yote yanayoushambulia mji wa Yerusalemu yatakuwa kama mtu mwenye njaa anayeota anakula lakini aamkapo bado anaumwa na njaa! Au mtu mwenye kiu anayeota kuwa anakunywa, lakini anaamka mdhaifu, bado ana kiu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakuwa kama mwenye njaa anayeota akila chakula, lakini anapoamka hakuna kitu kwake, au kama mwenye kiu anayeota akinywa, lakini anapoamka hutweta na kuivuta roho yake. Hivyo ndivyo, yatakavyokuwa mavumo ya wamizimu wote, waliokuja kuushambulia mlima wa Sioni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mataifa yote yanayoshambulia Yerusalema yatakuwa kama mutu mwenye njaa anayeota ndoto kwamba anakula lakini anaamuka angali bado na njaa, na kama mutu mwenye kiu anayeota kwamba anakunywa lakini anaamuka muzaifu, na angali bado na kiu.