Isaiah 29:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Endeleeni kuwa wapumbavu na kuduwaa! Jipofusheni na kuwa vipofu! Leweni lakini si kwa divai; pepesukeni lakini si kwa pombe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pigweni na butwaa na mshangae; jifanyeni vipofu wenyewe na msione; leweni, lakini si kwa mvinyo, pepesukeni lakini si kwa kileo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ngojeni mstaajabu; fanyeni anasa zenu na kuwa vipofu; wamelewa wala si kwa mvinyo; wamewaya-waya wala si kwa sababu ya kileo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Endeleeni kuwa wapumbavu na kuduwaa! Jipofusheni na kuwa vipofu! Leweni lakini si kwa divai; pepesukeni lakini si kwa pombe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Duwaa na kushangaa, jifanyeni vipofu wenyewe na msione, leweni, lakini si kwa mvinyo, pepesukeni lakini si kwa kileo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Duwaeni na kushangaa, jifanyeni vipofu wenyewe na msione, leweni, lakini si kwa mvinyo, pepesukeni lakini si kwa kileo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ngojeni mstaajabu; fanyeni anasa zenu na kuwa vipofu; wamelewa wala si kwa mvinyo; wamewayawaya wala si kwa sababu ya kileo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Endeleeni kuwa wapumbavu na kuduwaa! Jipofusheni na kuwa vipofu! Leweni lakini si kwa divai; pepesukeni lakini si kwa pombe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tumbueni macho na kuyakodoa! Yatieni giza na kupofuka! Wamelewa, lakini si kwa mvinyo, wanapepesuka, lakini si kwa kileo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ngojeni mstaajabu; fanyeni anasa zenu na kuwa vipofu; wamelewa wala si kwa mvinyo; wamewaya-waya wala si kwa sababu ya kileo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukuwe wapumbafu na kupumbazika: mupofuke na kuwa vipofu! Mulewe lakini si kwa divai; mupepesuke lakini si kwa pombe.