Isaiah 3:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema: “Wanawake wa Siyoni wana kiburi; wanatembea wameinua shingo juu, wakipepesa macho yao kwa tamaa. Hatua zao ni za maringo, na miguuni njuga zinalia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu asema, “Wanawake wa Sayuni wana kiburi, wanatembea na shingo ndefu, wakikonyeza kwa macho yao, wanatembea kwa hatua za madaha, wakiwa na mapambo ya njuga kwenye vifundo vya miguu yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema: “Wanawake wa Siyoni wana kiburi; wanatembea wameinua shingo juu, wakipepesa macho yao kwa tamaa. Hatua zao ni za maringo, na miguuni njuga zinalia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA asema, “Wanawake wa Sayuni wana kiburi, wanatembea na shingo ndefu, wakikonyeza kwa macho yao, wakitembea kwa hatua fupi fupi za madaha, wakiwa na mapambo yanayotoa mlio kwenye vifundo vya miguu yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana asema, “Wanawake wa Sayuni wana kiburi, wanatembea na shingo ndefu, wakikonyeza kwa macho yao, wanatembea kwa hatua za madaha, wakiwa na mapambo ya njuga kwenye vifundo vya miguu yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema: “Wanawake wa Siyoni wana kiburi; wanatembea wameinua shingo juu, wakipepesa macho yao kwa tamaa. Hatua zao ni za maringo, na miguuni njuga zinalia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana amesema: Kwa kuwa wanawake wa Sioni wamejikuza, wakatembea na kunyosha shingo na kutupia wengine macho yenye utongozi, wakienda na kuchezacheza na kuipigapiga mikufu ya miguu yao:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akasema tena, Kwa sababu binti za Sayuni wana kiburi, na kuenenda na shingo zilizonyoshwa, na macho ya kutamani, wakienenda kwa hatua za madaha, na kuliza njuga kwa miguu yao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema: Wanawake wa Sayuni wako na kiburi; wanatembea wakiinua kichwa juu, wakirembua macho yao kwa tamaa. Hatua zao ni za maringo, nao wanalilisha mikufu kwenye miguu yao.