Isaiah 3:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Badala ya kunukia marashi watatoa uvundo; badala ya mishipi mizuri watatumia kamba; badala ya nywele nzuri watakuwa na upara; badala ya mavazi mazuri watavaa matambara; uzuri wao wote utageuka kuwa aibu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Badala ya harufu ya manukato kutakuwa na uvundo; badala ya mishipi, ni kamba; badala ya nywele zilizotengenezwa vizuri, ni upara; badala ya mavazi mazuri, ni magunia; badala ya uzuri, ni alama ya aibu kwa chuma cha moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Badala ya kunukia marashi watatoa uvundo; badala ya mishipi mizuri watatumia kamba; badala ya nywele nzuri watakuwa na upara; badala ya mavazi mazuri watavaa matambara; uzuri wao wote utageuka kuwa aibu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Badala ya harufu ya manukato kutakuwa na uvundo; badala ya mishipi, kamba; badala ya nywele zilizotengenezwa vizuri, upara; badala ya mavazi mazuri, nguo za magunia; badala ya uzuri, alama ya aibu kwa chuma cha moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Badala ya harufu ya manukato kutakuwa na uvundo; badala ya mishipi, ni kamba; badala ya nywele zilizotengenezwa vizuri, ni upara; badala ya mavazi mazuri, ni nguo za magunia; badala ya uzuri, ni alama ya aibu kwa chuma cha moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Badala ya kunukia marashi watatoa uvundo; badala ya mishipi mizuri watatumia kamba; badala ya nywele nzuri watakuwa na upara; badala ya mavazi mazuri watavaa matambara; uzuri wao wote utageuka kuwa aibu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo penye manukato mazuri utakuwa mnuko wa kuoza, penye mikanda watapata kamba tu, penye misuko ya nywele patakuwa na vipara, penye zile nguo za urembo watajivika magunia, maumbufu matupu yatapashika mahali pa uzuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata itakuwa ya kuwa badala ya manukato mazuri kutakuwa uvundo, na badala ya mishipi, kamba; na badala ya nywele zilizosukwa vizuri, upaa; na badala ya kisibau, mavazi ya kigunia; na kutiwa alama mwilini kwa moto badala ya uzuri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa pahali pa harufu ya marasi watatoa uvundo; kwa pahali pa mikaba mizuri watatumia kamba; kwa pahali pa nywele nzuri watakuwa na upaa; kwa pahali pa nguo nzuri watavaa magunia; uzuri wao wote utageuka kuwa haya.