Isaiah 3:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini siku hiyo atasema, “Mimi siwezi kuwa mwuguzi, nyumbani mwangu hamna chakula wala mavazi. Msinifanye mimi kuwa kiongozi wenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini siku hiyo atapiga kelele akisema, “Sina msaada. Sina chakula wala mavazi katika nyumba yangu, msinifanye niwe kiongozi wa watu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi, siku ile atainua sauti yake, akisema, Mimi sitakuwa mponya watu; kwa maana ndani ya nyumba yangu hamna chakula wala mavazi; wala hamtanifanya kuwa mtawala juu ya watu hawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini siku hiyo atasema, “Mimi siwezi kuwa mwuguzi, nyumbani mwangu hamna chakula wala mavazi. Msinifanye mimi kuwa kiongozi wenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini siku hiyo atapiga kelele akisema, “Sina uponyaji. Sina chakula wala mavazi katika nyumba yangu, msinifanye niwe kiongozi wa watu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini siku hiyo atapiga kelele akisema, “Sina uponyaji. Sina chakula wala mavazi katika nyumba yangu, msinifanye niwe kiongozi wa watu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi, siku ile atainua sauti yake, akisema, Mimi sitakuwa mponya watu; kwa maana ndani ya nyumba yangu hamna chakula wala mavazi; wala hamtanifanya kuwa mtawala juu ya watu hawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini siku hiyo atasema, “Mimi siwezi kuwa mwuguzi, nyumbani mwangu hamna chakula wala mavazi. Msinifanye mimi kuwa kiongozi wenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye atajibu siku ileile na kupaza sauti: Mimi si mganga! Humu nyumbani mwangu hamna mkate wala nguo, msiniweke kuwa mwamuzi wenu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi, siku ile atainua sauti yake, akisema, Mimi sitakuwa mponya watu; kwa maana ndani ya nyumba yangu hamna chakula wala mavazi; wala hamtanifanya kuwa mtawala juu ya watu hawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini siku hiyo atasema: Mimi siwezi kuwa muponyaji. Ndani ya nyumba yangu hamuna chakula wala nguo. Musinifanye mimi kuwa mukubwa wenu.