Isaiah 3:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ubaguzi wao unashuhudia dhidi yao; wanatangaza dhambi yao kama ya Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao watu hao, kwani wamejiletea maangamizi wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nyuso zao zinavyoonekana zinashuhudia dhidi yao, hujivunia dhambi yao kama Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao! Wamejiletea maafa juu yao wenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ubaguzi wao unashuhudia dhidi yao; wanatangaza dhambi yao kama ya Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao watu hao, kwani wamejiletea maangamizi wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nyuso zao zinavyoonekana zinashuhudia dhidi yao, hujivunia dhambi yao kama Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao! Wamejiletea maafa juu yao wenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nyuso zao zinavyoonekana zinashuhudia dhidi yao, hujivunia dhambi yao kama Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao! Wamejiletea maafa juu yao wenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ubaguzi wao unashuhudia dhidi yao; wanatangaza dhambi yao kama ya Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao watu hao, kwani wamejiletea maangamizi wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ukorofi wa nyuso zao ukawaumbua, nao huyasimulia makosa yao pasipo kuyaficha kwa hivyo, wanavyofanana nao Wasodomu. Roho zao zitalipizwa vibaya, walivyojifanyizia wenyewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ubaguzi wao unashuhudia juu yao; wanatangaza zambi yao kama vile watu wa Sodoma, wala hawaifichi. Ole kwao watu hao, kwa sababu wamejiletea maangamizi wenyewe.