Isaiah 30:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Ole wao watoto wanaoniasi, wanaotekeleza mipango yao na si mipango yangu, wanaofanya mikataba kinyume cha matakwa yangu! Naam, wanarundika dhambi juu ya dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu asema, “Ole kwa watoto wakaidi, kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu, wakifanya makubaliano, lakini si kwa Roho wangu Mtakatifu, wakilundika dhambi juu ya dhambi,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wa watoto waasi; asema Bwana; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu; wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Ole wao watoto wanaoniasi, wanaotekeleza mipango yao na si mipango yangu, wanaofanya mikataba kinyume cha matakwa yangu! Naam, wanarundika dhambi juu ya dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA asema, “Ole wa watoto wakaidi, kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu, wakifanya umoja, lakini si kwa Roho wangu, wakilundika dhambi juu ya dhambi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana asema, “Ole kwa watoto wakaidi, kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu, wakifanya makubaliano, lakini si kwa Roho wangu, wakilundika dhambi juu ya dhambi,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wa watoto waasi; asema BWANA; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu; wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Ole wao watoto wanaoniasi, wanaotekeleza mipango yao na si mipango yangu, wanaofanya mikataba kinyume cha matakwa yangu! Naam, wanarundika dhambi juu ya dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Yatawapata wale wana wabishi wapigao shauri lisilo la kwangu, wafanyao agano pasipo Roho yangu, kusudi waongeze kosa kwa kosa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wa watoto waasi; asema BWANA; watakao mashauri lakini hawayataki kwangu mimi; wajifunikao kifuniko lakini si cha roho yangu; wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ole watoto waasi, wanaotimiza mipango yao na si mipango yangu, wanaofanya mapatano kinyume cha mapenzi yangu! –Ni ujumbe wa Yawe.– Kweli, wanalundika zambi juu ya zambi.