Isaiah 30:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuporomoka kwa ukuta huo, ni kama kupasuka kwa chungu ambacho kimepasuliwa vibaya sana, bila kusalia kigae cha kuchukulia moto mekoni, au kuchotea maji kisimani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utavunjika vipande vipande kama chombo cha udongo ukipasuka pasipo huruma ambapo katika vipande vyake hakuna kipande kitakachopatikana kwa kuukulia makaa kutoka jikoni au kuchotea maji kisimani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atapavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, akikivunja-vunja asiache kukivunja, hata hakipatikani katika vipande vyake kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, au kuteka maji kisimani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuporomoka kwa ukuta huo, ni kama kupasuka kwa chungu ambacho kimepasuliwa vibaya sana, bila kusalia kigae cha kuchukulia moto mekoni, au kuchotea maji kisimani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utavunjika vipande vipande kama chombo cha udongo ukipasuka pasipo huruma ambapo katika vipande vyake hakuna kipande kitakachopatikana kwa kuukulia makaa kutoka mekoni au kuchotea maji kisimani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utavunjika vipande vipande kama chombo cha udongo ukipasuka pasipo huruma ambapo katika vipande vyake hakuna kipande kitakachopatikana kwa kuukulia makaa kutoka jikoni au kuchotea maji kisimani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atapavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, kinavyovunjwavunjwa kikatili, hata hakipatikani katika vipande vyake kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, au kuteka maji kisimani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuporomoka kwa ukuta huo, ni kama kupasuka kwa chungu ambacho kimepasuliwa vibaya sana, bila kusalia kigae cha kuchukulia moto mekoni, au kuchotea maji kisimani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Bwana atauvunja, kama watu wanavyovunja mtungi wakiupigapiga pasipo kuuhurumia, hapo, utakapovunjika, kisipatikane kigae cha kupalia moto jikoni, wala cha kutekea maji kisimani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atapavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, akikivunja-vunja asiache kukivunja, hata hakipatikani katika vipande vyake kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, au kuteka maji kisimani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuporomoka kwa ukuta huo, ni kama kupasuka kwa chungu ambacho kimepasuliwa vibaya sana, bila kubaki kigae cha kuopolea moto ndani ya jiko, au kuchotea maji katika kisima.