Isaiah 30:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili, atainuka na kuwaonea huruma. Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki. Heri wote wale wanaomtumainia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo Mwenyezi Mungu anatamani kutupatia neema, anainuka ili kuwaonesha huruma. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu wa haki. Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa ajili ya hayo Bwana atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana Bwana ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili, atainuka na kuwaonea huruma. Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki. Heri wote wale wanaomtumainia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo BWANA anatamani kutupatia neema, anainuka ili kuwaonyesha huruma. Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa haki. Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo bwana anatamani kutupatia neema, anainuka ili kuwaonyesha huruma. Kwa kuwa bwana ni Mungu wa haki. Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili, atainuka na kuwaonea huruma. Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki. Heri wote wale wanaomtumainia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Bwana anangoja, apate kuwatolea upole; kwa hiyo anainuka, apate kuwahurumia, kwani Bwana ni Mungu wa kuamua kweli; wenye shangwe ni wote wanaomngoja,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata hivyo, Yawe anangoja kuwasamehe, atasimama na kuwaonea huruma. Yawe ni Mungu wa haki. Heri wote wale wanaomutumainia.