Isaiah 30:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtakapopanda mbegu zenu, Mwenyezi-Mungu atanyesha mvua kwa wakati wake, nazo zitakua na kuwapa mavuno mengi. Mifugo yenu nayo itapata malisho kwa wingi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia atawapa mvua kwa ajili ya mbegu mnazootesha ardhini, chakula kinachotoka ardhini kitakuwa kizuri sana, tena tele. Katika siku ile, ng’ombe wenu watalisha katika shamba pana la majani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atatoa mvua juu ya mbegu zako, upate kuipanda nchi hii; na mkate wa mazao ya nchi, nayo itasitawi na kuzaa tele; katika siku hiyo ng'ombe zako watakula katika malisho mapana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtakapopanda mbegu zenu, Mwenyezi-Mungu atanyesha mvua kwa wakati wake, nazo zitakua na kuwapa mavuno mengi. Mifugo yenu nayo itapata malisho kwa wingi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia atawapa mvua kwa ajili ya mbegu mnazootesha ardhini, chakula kinachotoka ardhini kitakuwa kizuri sana tena kwa wingi. Katika siku ile ng'ombe wenu watalisha katika shamba pana la majani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia atawapa mvua kwa ajili ya mbegu mnazootesha ardhini, chakula kinachotoka ardhini kitakuwa kizuri sana, tena tele. Katika siku ile, ng’ombe wenu watalisha katika shamba pana la majani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye atatoa mvua juu ya mbegu zako, upate kuipanda nchi hii; na mkate wa mazao ya nchi, nayo itasitawi na kuzaa tele; katika siku hiyo ng'ombe wako watakula katika malisho mapana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtakapopanda mbegu zenu, Mwenyezi-Mungu atanyesha mvua kwa wakati wake, nazo zitakua na kuwapa mavuno mengi. Mifugo yenu nayo itapata malisho kwa wingi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye atakupa mvua za mbegu zako, ulizozipanda shambani, nalo shamba litakutolea mikate itakayokuwa yenye nguvu ya kunonesha, nao kondoo wako watalisha siku zile kwenye uwanda mpana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atatoa mvua juu ya mbegu zako, upate kuipanda nchi hii; na mkate wa mazao ya nchi, nayo itasitawi na kuzaa tele; katika siku hiyo ng’ombe zako watakula katika malisho mapana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutakapopanda mbegu zenu, Yawe atanyesha mvua kwa wakati wake, nazo zitakomaa na kuwapa mavuno mengi mazuri. Makundi yenu ya nyama nao watakula katika mashamba makubwa ya kukulishia nyama.