Isaiah 30:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena mwezi utawaka kama jua, nao mwanga wa jua utakuwa mara saba ya mwanga wake wa kawaida, kana kwamba mwanga wa siku saba umeangaza katika siku moja. Mambo haya yote yatatukia wakati Mwenyezi-Mungu atakapoyafunga na kuyaponya majeraha aliyowaletea watu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwezi utaangaza kama jua, nao mwanga wa jua utang’aa mara saba zaidi, kama nuru ya siku saba, wakati Mwenyezi Mungu atakapoyafunga majeraha ya watu wake na kuwaponya vidonda alivyowatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile Bwana atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena mwezi utawaka kama jua, nao mwanga wa jua utakuwa mara saba ya mwanga wake wa kawaida, kana kwamba mwanga wa siku saba umeangaza katika siku moja. Mambo haya yote yatatukia wakati Mwenyezi-Mungu atakapoyafunga na kuyaponya majeraha aliyowaletea watu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwezi utaangaza kama jua, nao mwanga wa jua utang'aa mara saba zaidi, kama nuru ya siku saba, wakati BWANA atakapoyafunga majeraha ya watu wake na kuwaponya vidonda alivyowatia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwezi utaangaza kama jua, nao mwanga wa jua utang’aa mara saba zaidi, kama nuru ya siku saba, wakati bwana atakapoyafunga majeraha ya watu wake na kuwaponya vidonda alivyowatia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile BWANA atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha lao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena mwezi utawaka kama jua, nao mwanga wa jua utakuwa mara saba ya mwanga wake wa kawaida, kana kwamba mwanga wa siku saba umeangaza katika siku moja. Mambo haya yote yatatukia wakati Mwenyezi-Mungu atakapoyafunga na kuyaponya majeraha aliyowaletea watu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao mwanga wa mwezi utakuwa kama wa jua, nao mwanga wa jua utaongezeka mara saba, uwe kama wa siku saba. Itakuwa siku ile, Bwana atakapovifunga vidonda vyao walio ukoo wake na kuyaponya machubuko, aliyowapiga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile BWANA atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena mwezi utawaka kama jua, nao mwangaza wa jua utakuwa mara saba ya mwangaza wake wa kawaida, sawa vile kwamba mwangaza wa siku saba umeangaza katika siku moja. Mambo haya yote yatatukia wakati Yawe atakapofunga vidonda na kuponyesha mapigo aliyowaletea watu wake.