Isaiah 30:32 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila pigo la adhabu ya Mwenyezi-Mungu juu ya Waashuru litaandamana na mdundo wa ngoma na zeze. Yeye mwenyewe binafsi atapigana na Waashuru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila pigo Mwenyezi Mungu atakaloliweka juu yao kwa fimbo yake ya kuadhibu, litakuwa kwa wimbo wa matari na vinubi, anapopigana nao katika vita kwa mapigo ya mkono wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kila pigo la fimbo iliyoamriwa, ambayo Bwana ataliweka juu yake, litakuwa pamoja na matari na vinanda, na kwa mapigano yenye kutikisa atapigana nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila pigo la adhabu ya Mwenyezi-Mungu juu ya Waashuru litaandamana na mdundo wa ngoma na zeze. Yeye mwenyewe binafsi atapigana na Waashuru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila pigo BWANA atakaloliweka juu yao kwa fimbo yake ya kuadhibu, litakuwa kwa wimbo wa matari na vinubi, anapopigana nao katika vita kwa mapigo ya mkono wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila pigo bwana atakaloliweka juu yao kwa fimbo yake ya kuadhibu, litakuwa kwa wimbo wa matari na vinubi, anapopigana nao katika vita kwa mapigo ya mkono wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kila pigo la fimbo iliyoamriwa, ambayo BWANA ataliweka juu yake, litakuwa pamoja na matari na vinanda, na kwa mapigano yenye kutikisa atapigana nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila pigo la adhabu ya Mwenyezi-Mungu juu ya Waashuru litaandamana na mdundo wa ngoma na zeze. Yeye mwenyewe binafsi atapigana na Waashuru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kila mara fimbo ya kuwapiga itakapotokea, Bwana akiielekeza, iwajie, itakuwa kwa kupiga patu na mazeze, vita vyake vitakuwa hivyo akiwatisha na kuwapigapiga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kila pigo la fimbo iliyoamriwa, ambayo BWANA ataliweka juu yake, litakuwa pamoja na matari na vinanda, na kwa mapigano yenye kutikisa atapigana nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila pigo la azabu ya Yawe juu ya Waasuria litaandamana na mudundo wa ngoma na zeze. Yeye mwenyewe atapigana na Waasuria.