Isaiah 30:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naam, mahali pa kumteketeza mfalme wa Ashuru pamekwisha tayarishwa muda mrefu uliopita. Mahali penyewe ni shimo kubwa na pana. Moto upo na kuni kwa wingi. Mwenyezi-Mungu ataupulizia pumzi yake kama kijito cha madini ya kiberiti na kuuwasha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tofethi pameandaliwa toka zamani, pamewekwa tayari kwa ajili ya mfalme. Shimo lake la moto limetengenezwa kwa kina kirefu na kwa upana mkubwa, likiwa na moto na kuni tele; pumzi ya Mwenyezi Mungu, kama kijito cha kiberiti, huuwasha moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Tofethi imewekwa tayari tokea zamani, naam, imewekwa tayari kwa mfalme huyo; ameifanya kubwa, inakwenda chini sana; tanuru yake ni moto na kuni nyingi; pumzi ya Bwana, kama mto wa kiberiti, huiwasha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naam, mahali pa kumteketeza mfalme wa Ashuru pamekwisha tayarishwa muda mrefu uliopita. Mahali penyewe ni shimo kubwa na pana. Moto upo na kuni kwa wingi. Mwenyezi-Mungu ataupulizia pumzi yake kama kijito cha madini ya kiberiti na kuuwasha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tofethi imeandaliwa toka zamani, imewekwa tayari kwa ajili ya mfalme. Shimo lake la moto limetengenezwa kwa kina kirefu na kwa upana mkubwa, likiwa na moto na kuni tele; pumzi ya BWANA, kama kijito cha kiberiti, huuwasha moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tofethi imeandaliwa toka zamani, imewekwa tayari kwa ajili ya mfalme. Shimo lake la moto limetengenezwa kwa kina kirefu na kwa upana mkubwa, likiwa na moto na kuni tele; pumzi ya bwana, kama kijito cha kiberiti, huuwasha moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana Tofethi imewekwa tayari tokea zamani, naam, imewekwa tayari kwa mfalme huyo; ameifanya kubwa, inakwenda chini sana; tanuri yake ni moto na kuni nyingi; pumzi ya BWANA, kama mto wa kiberiti, huiwasha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naam, mahali pa kumteketeza mfalme wa Ashuru pamekwisha tayarishwa muda mrefu uliopita. Mahali penyewe ni shimo kubwa na pana. Moto upo na kuni kwa wingi. Mwenyezi-Mungu ataupulizia pumzi yake kama kijito cha madini ya kiberiti na kuuwasha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani tangu kale pametengenezwa mahali pa kuchinjia watu, wawe ng'ombe za tambiko, naye mfalme amepatengenezewa pake, napo ni papana na parefu kwenda chini; kuzunguka hapo moto uko tayari, hata kuni nyingi zimekwisha kupangwa; pumzi ya Bwana yenye moto wa kiberitiberiti itaziwasha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana Tofethi imewekwa tayari tokea zamani, naam, imewekwa tayari kwa mfalme huyo; ameifanya kubwa, inakwenda chini sana; tanuru yake ni moto na kuni nyingi; pumzi ya BWANA, kama mto wa kiberiti, huiwasha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kweli, pahali pa kumuteketeza mufalme wa Asuria pamekwisha kutayarishwa muda murefu uliopita. Pahali penyewe ni shimo kubwa na pana. Kuna moto na kuni kwa uwingi. Yawe ataupulizia pumzi yake kama kijito cha kiberiti na kuuwasha.