Isaiah 30:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kauli ya Mungu juu ya wanyama wa pande za Negebu: “Wajumbe wanapita katika nchi ya taabu na shida, yenye simba, nyoka wa sumu na majoka. Wamewabebesha wanyama wao mali zao, kuwapelekea watu wasioweza kuwafaa kitu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Neno la unabii kuhusu wanyama wa Negebu: Katika nchi ya taabu na shida, ya simba za dume na jike, ya nyoka mwenye sumu kali na nyoka warukao, wajumbe huchukua utajiri wao juu ya migongo ya punda, hazina zao juu ya nundu za ngamia, kwa lile taifa lisilokuwa na faida,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ufunuo juu ya hayawani wa Negebu. Katikati ya nchi ya taabu na dhiki, Ambayo hutoka huko simba jike na simba, Nyoka na joka la moto arukaye, Huchukua mali zao mabegani mwa punda wachanga, Na hazina zao juu ya nundu za ngamia Waende kwa watu ambao hawatawafaa kitu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kauli ya Mungu juu ya wanyama wa pande za Negebu: “Wajumbe wanapita katika nchi ya taabu na shida, yenye simba, nyoka wa sumu na majoka. Wamewabebesha wanyama wao mali zao, kuwapelekea watu wasioweza kuwafaa kitu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Neno kuhusu wanyama wa Negebu: Katika nchi ya taabu na shida, ya simba waume na wake, ya nyoka mwenye sumu kali na nyoka warukao, wajumbe huchukua utajiri wao juu ya migongo ya punda, hazina zao juu ya nundu za ngamia, kwa lile taifa lisilokuwa na faida,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Neno kuhusu wanyama wa Negebu: Katika nchi ya taabu na shida, ya simba za dume na jike, ya nyoka mwenye sumu kali na nyoka warukao, wajumbe huchukua utajiri wao juu ya migongo ya punda, hazina zao juu ya nundu za ngamia, kwa lile taifa lisilokuwa na faida,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ufunuo juu ya wanyama wa Negebu. Katikati ya nchi ya taabu na dhiki, Ambayo hutoka huko simba jike na simba angurumaye, Nyoka na joka la moto arukaye, Huchukua mali zao mabegani mwa punda wachanga, Na hazina zao juu ya nundu za ngamia Waende kwa watu ambao hawatawafaa kitu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kauli ya Mungu juu ya wanyama wa pande za Negebu: “Wajumbe wanapita katika nchi ya taabu na shida, yenye simba, nyoka wa sumu na majoka. Wamewabebesha wanyama wao mali zao, kuwapelekea watu wasioweza kuwafaa kitu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wanapita katika nchi yenye masongano na mahangaiko, kwani wamo simba na chui, pili na nyoka za moto warukao. Huko wanapitisha mali zao migongoni kwa punda, nako kwenye nundu za ngamia malimbiko yao, wayapelekee watu wasiowafalia kitu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ufunuo juu ya hayawani wa Negebu. Katikati ya nchi ya taabu na dhiki, Ambayo hutoka huko simba jike na simba, Nyoka na joka la moto arukaye, Huchukua mali zao mabegani mwa punda wachanga, Na hazina zao juu ya nundu za ngamia Waende kwa watu ambao hawatawafaa kitu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ujumbe wa Mungu juu ya nyama wa pande za jangwa ya kusini: Wajumbe wanapita katika inchi ya taabu na shida, yenye simba, nyoka wa sumu na nyoka wakubwa wanaoruka. Wamewabebesha punda na ngamia wao mali zao, kuwapelekea watu wasioweza kuwafalia kitu.