Isaiah 31:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ole wao wale waendao Misri kuomba msaada, ole wao wanaotegemea farasi, wanaotegemea wingi wa magari yao ya vita, na nguvu za askari wao wapandafarasi, nao hawamtegemei Mtakatifu wa Israeli, wala hawamwombi Mwenyezi-Mungu shauri!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ole wao wale wanaoshuka Misri kutafuta msaada, wale wanaotegemea farasi, wanaoweka tumaini katika wingi wa magari yao ya vita, na katika nguvu nyingi za wapanda farasi, lakini hawamwangalii yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, wala hawatafuti msaada kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wao watelemkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti Bwana!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ole wao wale waendao Misri kuomba msaada, ole wao wanaotegemea farasi, wanaotegemea wingi wa magari yao ya vita, na nguvu za askari wao wapandafarasi, nao hawamtegemei Mtakatifu wa Israeli, wala hawamwombi Mwenyezi-Mungu shauri!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ole wao wale washukao Misri kwa ajili ya msaada, wale wategemeao farasi, wanaoweka tumaini katika wingi wa magari yao ya vita na katika nguvu nyingi za wapanda farasi, lakini hawamwangalii yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, wala hawatafuti msaada kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ole wao wale washukao Misri kwa ajili ya msaada, wale wategemeao farasi, wanaoweka tumaini katika wingi wa magari yao ya vita, na katika nguvu nyingi za wapanda farasi, lakini hawamwangalii yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, wala hawatafuti msaada kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wao wateremkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti BWANA!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ole wao wale waendao Misri kuomba msaada, ole wao wanaotegemea farasi, wanaotegemea wingi wa magari yao ya vita, na nguvu za askari wao wapandafarasi, nao hawamtegemei Mtakatifu wa Israeli, wala hawamwombi Mwenyezi-Mungu shauri!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatawapata washukao kwenda Misri kutafuta msaada, wakijishikiza kwa farasi, wakaegemea magari, kwamba ni mengi, hata wapanda farasi, kwamba ni wenye nguvu sana, lakini hawakumtazamia Mtakatifu wa Isiraeli, Bwana hawakumtafuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wao watelemkao kwenda Misri wapate msaada, na kutegemea farasi; watumainio magari kwa kuwa ni mengi, na wapanda farasi kwa kuwa ni hodari sana; lakini hawamwangalii Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti BWANA!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ole kwao wale wanaokwenda Misri kuomba musaada! Wanategemea farasi, wanategemea wingi wa magari ya vita na nguvu za waaskari wao wapanda-farasi. Lakini hawamutegemei Mutakatifu wa Israeli, wala hawamwombi Yawe shauri!