Isaiah 31:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Kama vile simba au mwanasimba angurumavyo kuyakinga mawindo yake, hata kundi la wachungaji likiitwa kumkabili, yeye hatishiki kwa kelele zao, wala hashtuki kwa sauti zao. Ndivyo atakavyoshuka Mwenyezi-Mungu wa majeshi kupigana juu ya mlima Siyoni na kilima chake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo Mwenyezi Mungu analoniambia: “Kama vile simba angurumavyo, simba mkubwa juu ya mawindo yake: hata ingawa kundi lote la wafugaji huitwa pamoja dhidi yake, hatiwi hofu na kelele zao, wala kusumbuliwa na ghasia zao; ndivyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni atakavyoshuka kufanya vita juu ya Mlima Sayuni na juu ya vilele vyake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana aniambia hivi, Kama vile ilivyo simba angurumapo na mwana-simba juu ya mawindo yake, wachungaji wengi wakiitwa ili kumpiga, lakini hatiwi hofu na sauti zao, wala kufanya woga kwa sababu ya mshindo wao; ndivyo Bwana wa majeshi atakavyoshuka ili kufanya vita juu ya mlima Sayuni, na juu ya kilima chake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Kama vile simba au mwanasimba angurumavyo kuyakinga mawindo yake, hata kundi la wachungaji likiitwa kumkabili, yeye hatishiki kwa kelele zao, wala hashtuki kwa sauti zao. Ndivyo atakavyoshuka Mwenyezi-Mungu wa majeshi kupigana juu ya mlima Siyoni na kilima chake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo BWANA analoniambia: “Kama vile simba angurumavyo, simba mkubwa juu ya mawindo yake: hata ingawa kundi lote la wachunga mifugo huitwa pamoja dhidi yake, hatiwi hofu na kelele zao wala kusumbuliwa na ghasia zao; ndivyo BWANA Mwenye Nguvu Zote atakavyoshuka kufanya vita juu ya Mlima Sayuni na juu ya vilele vyake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo bwana analoniambia: “Kama vile simba angurumavyo, simba mkubwa juu ya mawindo yake: hata ingawa kundi lote la wachunga mifugo huitwa pamoja dhidi yake, hatiwi hofu na kelele zao wala kusumbuliwa na ghasia zao; ndivyo bwana Mwenye Nguvu Zote atakavyoshuka kufanya vita juu ya Mlima Sayuni na juu ya vilele vyake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA aniambia hivi, Kama vile ilivyo simba angurumapo na mwanasimba juu ya mawindo yake, wachungaji wengi wakiitwa ili kumpiga, lakini hatiwi hofu na sauti zao, wala kufanya woga kwa sababu ya mshindo wao; ndivyo BWANA wa majeshi atakavyoshuka ili kufanya vita juu ya mlima Sayuni, na juu ya kilima chake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Kama vile simba au mwanasimba angurumavyo kuyakinga mawindo yake, hata kundi la wachungaji likiitwa kumkabili, yeye hatishiki kwa kelele zao, wala hashtuki kwa sauti zao. Ndivyo atakavyoshuka Mwenyezi-Mungu wa majeshi kupigana juu ya mlima Siyoni na kilima chake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, Bwana alivyoniambia: Itakuwa kama simba au mwana wa simba, akikamata kondoo na kunguruma; kisha wachungaji wakiitana wengi, wamnyang'anye, hazistukii sauti zao, wala hatishiki kwa makelele yao; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi atakavyoshuka kupiga vita, mlimani kwa Sioni nako kwenye kilima chake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA aniambia hivi, Kama vile ilivyo simba angurumapo na mwana-simba juu ya mawindo yake, wachungaji wengi wakiitwa ili kumpiga, lakini hatiwi hofu na sauti zao, wala kufanya woga kwa sababu ya mshindo wao; ndivyo BWANA wa majeshi atakavyoshuka ili kufanya vita juu ya mlima Sayuni, na juu ya kilima chake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe aliniambia hivi: Simba mukali ananguruma kwa kukinga nyama aliyemukamata; hata kundi la wachungaji likiitwa kwa kumufukuza, hatishiki kwa kelele zao, wala hashituki kwa sauti zao. Ni vile Yawe wa majeshi atakavyoshuka kupigana juu ya mulima Sayuni na kilima chake.