Isaiah 31:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Waashuru watauawa kwa upanga, lakini si kwa upanga wa binadamu; naam, wataangamizwa kwa upanga ambao ni zaidi ya ule wa binadamu. Waashuru watakimbia na vijana wao watafanyizwa kazi za kitumwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ashuru itaanguka kwa upanga ambao si wa mwanadamu; upanga usio wa kibinadamu utawaangamiza. Watakimbia mbele ya upanga na vijana wao wa kiume watafanyizwa kazi kwa lazima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamla; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Waashuru watauawa kwa upanga, lakini si kwa upanga wa binadamu; naam, wataangamizwa kwa upanga ambao ni zaidi ya ule wa binadamu. Waashuru watakimbia na vijana wao watafanyizwa kazi za kitumwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ashuru itaanguka kwa upanga ambao si wa mwanadamu; upanga, ambao si wa kibinadamu, utawaangamiza. Watakimbia mbele ya upanga na vijana wao wa kiume watafanyizwa kazi kwa lazima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ashuru itaanguka kwa upanga ambao si wa mwanadamu; upanga usio wa kibinadamu utawaangamiza. Watakimbia mbele ya upanga na vijana wao wa kiume watafanyizwa kazi kwa lazima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamwangamiza; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Waashuru watauawa kwa upanga, lakini si kwa upanga wa binadamu; naam, wataangamizwa kwa upanga ambao ni zaidi ya ule wa binadamu. Waashuru watakimbia na vijana wao watafanyizwa kazi za kitumwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Waasuri watakapouawa kwa panga zisizo za waume, kweli panga zitawala, lakini sizo za watu; hizo panga watazikimbia, nao vijana wao watakuwa watumwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamla; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo Waasuria watauawa kwa upanga, lakini si upanga wa watu; wataangamizwa kwa upanga ambao ni zaidi ya ule wa wanadamu. Waasuria watakimbia na vijana wao watatumikishwa kazi za kitumwa.