Isaiah 32:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wapumbavu hunena upumbavu, na fikira zao hupanga kutenda uovu, kutenda mambo yasiyo mema, kusema mambo ya kumkufuru Mwenyezi-Mungu. Huwaacha wenye njaa bila chakula, na wenye kiu huwanyima kinywaji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu, moyo wake hushughulika na uovu: Hutenda mambo yasiyo ya kumcha Mungu, na hueneza habari za makosa kuhusu Mwenyezi Mungu; yeye huwaacha wenye njaa bila kitu, na wenye kiu huwanyima maji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mpumbavu atanena yaliyo upumbavu, na moyo wake utafanya maovu, ili kutenda hila na kusema yasiyo kweli juu ya Bwana, ili kuziacha nafsi za watu wenye njaa hazina kitu, na kukikomesha kinywaji chake mwenye kiu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wapumbavu hunena upumbavu, na fikira zao hupanga kutenda uovu, kutenda mambo yasiyo mema, kusema mambo ya kumkufuru Mwenyezi-Mungu. Huwaacha wenye njaa bila chakula, na wenye kiu huwanyima kinywaji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu, moyo wake hushughulika na uovu: Hutenda mambo yasiyo ya uchaji Mungu, na hueneza habari za makosa kuhusu BWANA; yeye huwaacha wenye njaa bila kitu na wenye kiu huwanyima maji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu, moyo wake hushughulika na uovu: Hutenda mambo yasiyo ya kumcha Mungu, na hueneza habari za makosa kuhusu bwana; yeye huwaacha wenye njaa bila kitu, na wenye kiu huwanyima maji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mpumbavu atanena yaliyo upumbavu, na moyo wake utafanya maovu, ili kutenda hila na kusema yasiyo kweli juu ya BWANA, ili kuziacha nafsi za watu wenye njaa bila chakula, na kuwanyima kinywaji wenye kiu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wapumbavu hunena upumbavu, na fikira zao hupanga kutenda uovu, kutenda mambo yasiyo mema, kusema mambo ya kumkufuru Mwenyezi-Mungu. Huwaacha wenye njaa bila chakula, na wenye kiu huwanyima kinywaji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mjinga husema yenye ujinga, nao moyo wake hufanya maovu: hufanya yaliyo machafu machoni pake Bwana, tena husema maneno ya kupoteza watu, wasimjie Bwana, mwenye njaa humwacha, akae vivyo hivyo na njaa yake, naye mwenye kiu humnyima cha kunywa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mpumbavu atanena yaliyo upumbavu, na moyo wake utafanya maovu, ili kutenda hila na kusema yasiyo kweli juu ya BWANA, ili kuziacha nafsi za watu wenye njaa hazina kitu, na kukikomesha kinywaji chake mwenye kiu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wapumbafu wanasema maneno ya upumbafu, na mafikiri yao ni kutenda maovu, kutenda mambo ya watu wasiomujua Mungu, kusema maneno ya kumutukana Yawe. Wanawaacha wenye njaa bila chakula, na wenye kiu wanawanyima kinywaji.