Isaiah 32:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ulaghai wa walaghai ni mbaya; hao huzua visa viovu, na kumwangamiza maskini kwa maneno ya uongo, hata kama madai ya maskini ni halali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu, hufanya mipango miovu ili kumwangamiza maskini kwa uongo, hata wakati hoja za mhitaji ni za haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena vyombo vyake ayari ni vibaya; hutunga hila mbaya, ili kuwaangamiza wanyonge kwa maneno ya uongo, mtu mhitaji ajaposema maneno yenye haki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ulaghai wa walaghai ni mbaya; hao huzua visa viovu, na kumwangamiza maskini kwa maneno ya uongo, hata kama madai ya maskini ni halali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu, hufanya mipango miovu ili kumwangamiza maskini kwa uongo, hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu, hufanya mipango miovu ili kumwangamiza maskini kwa uongo, hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena vyombo vyake mlaghai ni vibaya; hutunga hila mbaya, ili kuwaangamiza wanyonge kwa maneno ya uongo, mtu mhitaji ajaposema maneno yenye haki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ulaghai wa walaghai ni mbaya; hao huzua visa viovu, na kumwangamiza maskini kwa maneno ya uongo, hata kama madai ya maskini ni halali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mdanganyifu mizungu yake ni mibaya: huwaza njia za kupotoa, apate kuangamiza wanyonge kwa maneno ya uwongo, ijapo mkiwa aseme yanyokayo shaurini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena vyombo vyake ayari ni vibaya; hutunga hila mbaya, ili kuwaangamiza wanyonge kwa maneno ya uongo, mtu mhitaji ajaposema maneno yenye haki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Matendo ya watu wadanganyifu ni mabaya; hao wanatunga maneno mabaya kwa kumwangamiza masikini kwa maneno ya uongo, hata kama masikini ni mwenye sheria.