Isaiah 33:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ole wako ewe mwangamizi, unayeangamiza bila wewe kuangamizwa! Ole wako wewe mtenda hila, ambaye hakuna aliyekutendea hila! Utakapokwisha kuangamiza wewe utaangamizwa! Utakapomaliza kuwatendea watu hila wewe utatendewa hila.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ole wako wewe, ee mharibu, wewe ambaye hukuharibiwa! Ole wako, ee msaliti, wewe ambaye hukusalitiwa! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa; utakapokwisha kusaliti, utasalitiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendaye hila wala hukutendwa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe; na utakapokwisha kutenda kwa hila, wao watakutenda hila wewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ole wako ewe mwangamizi, unayeangamiza bila wewe kuangamizwa! Ole wako wewe mtenda hila, ambaye hakuna aliyekutendea hila! Utakapokwisha kuangamiza wewe utaangamizwa! Utakapomaliza kuwatendea watu hila wewe utatendewa hila.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ole wako wewe, Ee mharabu, wewe ambaye hukuharibiwa! Ole wako, Ee msaliti, wewe ambaye hukusalitiwa! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa; utakapokwisha kusaliti, utasalitiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ole wako wewe, ee mharabu, wewe ambaye hukuharibiwa! Ole wako, ee msaliti, wewe ambaye hukusalitiwa! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa; utakapokwisha kusaliti, utasalitiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendaye hila wala hukutendwa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe; na utakapokwisha kutenda kwa hila, wao watakutenda hila wewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ole wako ewe mwangamizi, unayeangamiza bila wewe kuangamizwa! Ole wako wewe mtenda hila, ambaye hakuna aliyekutendea hila! Utakapokwisha kuangamiza wewe utaangamizwa! Utakapomaliza kuwatendea watu hila wewe utatendewa hila.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenye kuapizwa ni wewe mkorofi usiyekorofishwa bado, mwenye kuapizwa ni wewe mpokonyi usiyepokonywa bado. Utakapomaliza kukorofisha utakorofishwa, utakapomaliza kupokonya utapokonywa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wako uharibuye ila hukuharibiwa, utendaye hila wala hukutendwa hila! Utakapokwisha kuharibu, utaharibiwa wewe; na utakapokwisha kutenda kwa hila, wao watakutenda hila wewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ole kwako! Unaangamiza ingawa hauangamizwi. Unadanganya ingawa haudanganywi. Utakapokwisha kuangamiza, wewe utaangamizwa! Utakapomaliza kudanganya, wewe utadanganywa.