Isaiah 33:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wenye dhambi katika Siyoni wanaogopa, wasiomcha Mungu wanatetemeka na kusema: “Nani awezaye kuukaribia moto huu mkali? Nani awezaye kustahimili miali ya moto wa milele?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu, kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu: “Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao? Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wenye dhambi katika Siyoni wanaogopa, wasiomcha Mungu wanatetemeka na kusema: “Nani awezaye kuukaribia moto huu mkali? Nani awezaye kustahimili miali ya moto wa milele?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu, kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu: “Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao? Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu, kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu: “Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao? Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uangamizao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wenye dhambi katika Siyoni wanaogopa, wasiomcha Mungu wanatetemeka na kusema: “Nani awezaye kuukaribia moto huu mkali? Nani awezaye kustahimili miali ya moto wa milele?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakosaji walioko Sioni wamestuka, tetemeko likawashika wapotovu, wakasema: Kwetu sisi yuko nani awezaye kukaa penye moto ulao? Kwetu sisi yuko nani awezaye kukaa penye majiko yasiyozima kale na kale?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto ulao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wenye zambi katika Sayuni wanaogopa, wasiomwamini Mungu wanatetemeka na kusema: Nani anayeweza kuvumilia moto huu mukali? Nani anayeweza kuvumilia ndimi za moto usiozimika?