Isaiah 33:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni mtu aishiye kwa uadilifu na asemaye ukweli; mtu anayedharau kabisa utajiri wa dhuluma, anayekataa hongo kata kata, asiyekubali kamwe kusikia mipango ya mauaji, wala hakubali macho yake yaone maovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye aendaye kwa uadilifu na kusema lililo haki, yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma na kuizuia mikono yake isipokee rushwa, yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji, na yeye afumbaye macho yake yasitazame uovu:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung'utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni mtu aishiye kwa uadilifu na asemaye ukweli; mtu anayedharau kabisa utajiri wa dhuluma, anayekataa hongo kata kata, asiyekubali kamwe kusikia mipango ya mauaji, wala hakubali macho yake yaone maovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye aendaye kwa uadilifu na kusema lile lililo sawa, yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma na kuizuia mikono yake isipokee rushwa, yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye aendaye kwa uadilifu na kusema lililo haki, yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma na kuizuia mikono yake isipokee rushwa, yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji, na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung'utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za umwagaji wa damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni mtu aishiye kwa uadilifu na asemaye ukweli; mtu anayedharau kabisa utajiri wa dhuluma, anayekataa hongo kata kata, asiyekubali kamwe kusikia mipango ya mauaji, wala hakubali macho yake yaone maovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni yeye aendeleaye kwa wongofu naye asemaye yanyokayo, naye akataaye mapato ya ukorofi naye akung'utaye mikono yake, isishike mapenyezo, naye ayazibaye masikio yake, asisikie mashauri ya damu zilizomwagwa, naye ayafumbaye macho yake, asiyaone mabaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung’utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni mutu anayekuwa hivi: anaishi kwa haki na kusema kwa usawa, anazarau kabisa utajiri wa unyanganyi, anakataa kupokea kituliro, hakubali hata kidogo kusikia mipango ya mauaji, wala hakubali macho yake yaone maovu.