Isaiah 33:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tazameni Siyoni tunamofanya sikukuu zetu; tazameni mji Yerusalemu, makao matulivu, hema imara; vigingi vyake havitangolewa kamwe, kamba zake hazitakatwa hata moja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtazame Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yenu yatauona Yerusalemu, mahali pa amani pa kuishi, hema ambalo halitaondolewa, nguzo zake hazitang’olewa kamwe, wala hakuna kamba yake yoyote itakayokatika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa kao la raha; hema isiyotanga-tanga; vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tazameni Siyoni tunamofanya sikukuu zetu; tazameni mji Yerusalemu, makao matulivu, hema imara; vigingi vyake havitang'olewa kamwe, kamba zake hazitakatwa hata moja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtazame Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yenu yatauona Yerusalemu, mahali pa amani pa kuishi, hema ambalo halitaondolewa, nguzo zake hazitang'olewa kamwe, wala hakuna kamba yake yo yote itakayokatika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtazame Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yenu yatauona Yerusalemu, mahali pa amani pa kuishi, hema ambalo halitaondolewa, nguzo zake hazitang’olewa kamwe, wala hakuna kamba yake yoyote itakayokatika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa makao ya raha; hema isiyotikisika; vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tazameni Siyoni tunamofanya sikukuu zetu; tazameni mji Yerusalemu, makao matulivu, hema imara; vigingi vyake havitangolewa kamwe, kamba zake hazitakatwa hata moja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Utazameni Sioni ule mji wetu wa kukusanyikiamo! Macho yako yataona, ya kuwa Yerusalemu ni kao lisilosumbua, ni hema lisilosafiri, mambo zake hazing'olewi kale na kale, kamba zake zote hazikatiki kamwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa kao la raha; hema isiyotanga-tanga; vigingi vyake havitang’olewa, wala kamba zake hazitakatika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muangalie Sayuni tunamofanyia sikukuu zetu; muangalie Yerusalema, makao matulivu, hema imara; misumari yake haitaongolewa hata kidogo, kamba zake hazitakatwa hata moja.