Isaiah 33:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maadui zao wanakusanya mateka, wanayarukia kama panzi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mateka yenu, enyi mataifa, yamevunwa kama wafanyavyo madumadu, watu huvamia juu yake kama kundi la nzige.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mateka yako yatakumbwa kama wadudu wakumbavyo, wataruka juu yake kama arukavyo nzige.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maadui zao wanakusanya mateka, wanayarukia kama panzi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mateka yako, Enyi mataifa, yamevunwa kama vile wafanyavyo madumadu, kama kundi la nzige watu huvamia juu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mateka yenu, enyi mataifa, yamevunwa kama vile wafanyavyo madumadu, kama kundi la nzige watu huvamia juu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mateka yako yatakusanywa kama wadudu wakumbavyo, wataruka juu yake kama arukavyo nzige.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maadui zao wanakusanya mateka, wanayarukia kama panzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mateka yenu yatakapookotwa, kama watu wanavyookota nzige; kama funutu wanavyojikimbilia, ndivyo, watakavyojikimbilia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mateka yako yatakumbwa kama wadudu wakumbavyo, wataruka juu yake kama arukavyo nzige.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waadui zao wanakusanya vitu walivyonyanganya, wanavirukia kama mapanzi.