Isaiah 33:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Barabara kuu zimebaki tupu; hamna anayesafiri kupitia humo. Mikataba inavunjwa ovyo, mashahidi wanadharauliwa. Hamna anayejali tena maisha ya binadamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Njia kuu zimeachwa, hakuna wasafiri barabarani. Mkataba umevunjika, mashahidi wake wamedharauliwa, hakuna anayeheshimiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Njia kuu zimeachwa, msafiri amekoma; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Barabara kuu zimebaki tupu; hamna anayesafiri kupitia humo. Mikataba inavunjwa ovyo, mashahidi wanadharauliwa. Hamna anayejali tena maisha ya binadamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Njia kuu zimeachwa, hakuna wasafiri barabarani. Mkataba umevunjika, mashahidi wake wamedharauliwa, hakuna ye yote anayeheshimiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Njia kuu zimeachwa, hakuna wasafiri barabarani. Mkataba umevunjika, mashahidi wake wamedharauliwa, hakuna yeyote anayeheshimiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Njia kuu zimeachwa, msafiri ameikimbia barabara; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Barabara kuu zimebaki tupu; hamna anayesafiri kupitia humo. Mikataba inavunjwa ovyo, mashahidi wanadharauliwa. Hamna anayejali tena maisha ya binadamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Barabara ziko peke yao, hakuna apitaye njiani. Amevunja agano kwa kuibeza miji na kwa kuwawazia watu kuwa si kitu. Nchi inazimia kwa kusikitika:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Njia kuu zimeachwa, msafiri amekoma; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Barabara kubwa zimebaki tupu; hakuna anayesafiri kupitia ndani yao. Mapatano yanavunjwa ovyo, washuhuda wanazarauliwa. Hakuna anayejali tena maisha ya wanadamu.